• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kibaha Town Council
Kibaha Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Kibaha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto
      • Ujenzi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mazingira na Mipango Miji
      • UKIMWI
      • Maadili
      • Ustawi wa Jamii
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Viombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Maendeleo ya Jamii

MAJUKUMU YA KAZI ZA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII

Idara kwa ujumla inalo jukumu la kushirikisha jamii katika suala zima la kuondoa umaskini kwa kuiwezesha jamii kubaini matatizo yao, kupanga mipango yao, kutekeleza na kutathmini utekelezaji wa shughuli zao, kwa kutumia rasilimali zilizomo kwenye mazingira yao. Ikibidi kushirikisha juhudi za wengine, zikiwemo za Serikali, wahisani mbalimbali, lakini ushiriki wa jamii yenyewe ni muhimu zaidi ili kuwaletea maendeleo endelevu.

  1. Kuratibu shughuli za wanawake na watoto
  2. Kutoa mikopo na kufuatilia marejesho kwa vikundi vya wanawake na vijana
  3. Kufanya maadhimisho mbalimbali
    1. Siku ya wanawake Dunuani
    2. Siku ya mtoto wa Afrika
    3. Siku ya Mtoto wa kike
    4. Siku ya UKIMWI Duniani
    5. Siku ya Familia duniani
  4. Kuhamasishaji wa Jamii katika utekelezaji wa Miradi ya maji
  5. Kufanya mikutano ya kuamsha ari kwa jamii.
  6. Kuratibu shughuli za Dawati la Malalamiko
  7. Kuratibu na Kusajili  Asasi za kiraia
  8. Kuratibu wa  shughuli za Vijana.
  9. Kuratibu uwezeshaji wa wananchi kiuchumi
  10. Kushughulikia masuala ya Kitengo cha Ustawi wa jamii
  11. Kuratibu shughuli za TASAF kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini

UTEKELEZAJI KIPINDI CHA ROBO YA TATU MWAKA 2017/18

Uwezeshaji wananchi kiuchumi

Pamoja na majukumu ya kawaida Idara imeweza kufuatilia marejesho ya vikundi 108 vya wanawake vilivyopewa mkopo na riba TShs.  279,950,000/= iliyowanufaisha wanawake 805. Vikundi imeweza kurejesha Tshs: 120,305,000/= sawa na asilimia 43. Vikundi vya vijana kupitia SACCOS vimepewa mikopo ya Tshs. 20,000,000/= na kuweza kurejesha Tshs. 12,000,000/= baki Tshs. 8,000,000/=. Jumla ya form 93 zimegawiwa za kujiunga na Program ya VIA- jiandalie ajira kwa kushirikiana na Taasisi ya ujasiriamali (TECC) Tanzania Entrepreneurship and Competative Centre. Idara pia imepokea Tshs 19,000,000 kwa ajili ya kuvikopesha vikundi 2 vya vikundi ya vijana vya Rabit Farm na Peace Fish production toka katika  Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF)

Uratibu wa asasi za kijamii

Idara imeratibu na kusajili asasi za kijamii 86. Asasi hizo zimeweza kutoa huduma mbalimbali kwa jamii zikiwemo za;-

  • Mafunzo Wahamasishaji 24 wa Afya Majumbani
  • Hatua za upangaji wa Mipango ya Maendeleo kwa kadri ya miongozo ya Halmashauri watu 1800 (Ke 1100 na Me 700) wamefikiwa kwa njia ya vipeperushi
  • Wanawake 65 wamepata mafunzo juu ya umiliki wa ardhi.

Uratibu wa viwanda

Idara imeendelea na uratibu na uhamasishaji wa uanzishwaji wa viwanda vidogo na vya kati. Hadi sasa takwimu za viwanda vidogo 88 zimekusanywa. Viwanda hivi vinajishughulisha na Ubanguaji korosho, utengenezaji wa sabuni, batiki, uchomeaji vyuma, usindikaji wa vyakula, kutengeneza grisi, viatu na vifungashio

Kuamsha ari kwa jamii

Zoezi la kuamsha ari limefanyika katika Mitaa 7 iliyopo katika Kata 5 yenye miradi ya ujenzi wa zahanati, madarasa na vyoo vya shule za msingi. Wananchi wanaonyesha kuwa wana ari ya kushiriki na kuchangia utekelezaji wa miradi yao.

Maadhimisho ya siku ya wanawake dunuani

Siku ya wanawake duniani mwaka 2018 imeadhimishwa katika Kata ya Kibaha, Mtaa wa Mwendapole A. Kauli mbiu ya mwaka 2018 ilikuwa,  “Kuelekea  Uchumi wa Viwanda: Tuimarishe Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji Wanawake Vijijini’’.  Maadhimisho yaliambatana maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na viwanda vidogo na vya  kati vya wanawake wajasirimali.

Uhamasishaji jamii miradi ya maji

Uhamasishaji jamii katika utekelezaji wa miradi ya Maji umefanyika ambapo jamii imeunda vyombo vya watumia maji (COWSO) katika maeneo ya Sofu, Kalabaka, Muheza na Kidugalo ambapo uchaguzi wa viongozi wa vituo vya kuchotea maji umekamilika na uchaguzi wa viongozi wa jumuiya wameishachaguliwa.

Uratibu wa dawati la malalamiko

Dawati la malalamiko limepokea malalamiko kumi (10) kutoka Serikali ya Mtaa wa Mkuza, Idara ya Ardhi ihusuyo migogoro ya Ardhi, Idara ya maji (DAWASCO) kutoka Mtaa wa Uyaoni  na Idara ya Maendeleo ya Jamii  kuhusiana na Ajira kwa Vijana Viwandani. Malalamiko 2 kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii na moja kutoka Idara ya Maji (DAWASCO) yamepatiwa ufumbuzi (yamekamilika)         na yaliyobaki yapo kwenye vitengo husika yanashughulikiwa.

Uratibu wa shughuli za TASAF

Utekelezaji wa shughuli za TASAF kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini katika robo ya tatu 2017/18 umezipatia fedha kaya masikini (walengwa) 2,136. Lengo ni kuzipatia kaya masikini ruzuku ya masharti na ruzuku isiyo na masharti ambapo walengwa hupatiwa ruzuku ya miezi miwili miwili kati ya Tshs. 20,000 na Tshs. 70,000 kulingana na ukubwa wa kaya na idadi ya wanakaya.

Aidha baadhi ya walengwa wameonyesha kuwa na mafanikio kwa kuboresha  hali za maisha yao ambapo wameweza kuanzisha biashara ndogondogo, ufugaji, kilimo na kuboresha maisha.

Imeandaliwa na

Leah Lwanji

Afisa Maendeleo ya Jamii Mji

Halmashauri ya Mji Kibaha.


Matangazo

  • INEC yahimiza Wananchi mikoa 16 kujitokeza uboreshaji Daftari awamu ya pili May 14, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUND VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 02, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -MSAIDIZI KUMBUKUMBU II October 06, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA WA TAKUKURU WATOA ELIMU YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MJI KIBAHA

    June 10, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZA UPASUAJI ZAANZA HOSPITALI YA LULANZI

    May 27, 2025
  • MWENYEKITI WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHUGUZI , Mhe. JAJI WA RUFAA JACOBS MWAMBEGELE LEO MEI 14,2025 AMETEMBELEA NA KUZUNGUMZA NA WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.

    May 14, 2025
  • ZOEZI LA MABORESHO YA DAFTARI LA WAPIGA KURA KUANZA MEI 16 KIBAHA TC

    May 09, 2025
  • Tazama Zote

Video

Mh. Waziri Mkuu akiwa ziarani Kibaha
Picha za Kutembea

Kiungo cha Haraka

  • Sheria Ndogo(Ushuru wa magari ya abiria na mizigo)
  • Barua Pepe
  • Uujazi wa Viwanja
  • Muundo Wa Kiuongozi Halmashauri
  • Dira na Dhamira ya Halmashauri

Kiungo Kinachohusiana

  • Mkoa wa Pwani
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Ofisi ya Raisi, Tawala za Serikali za Mikoa na Mitaa
  • Utumishi
  • Utumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani Ilipo

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera za Siri
    • Disclamer
    • MMM
    • Sitemap
    • Huduma

Haki Zote Zimahifadhiwa